Pages

Monday, 13 March 2023

FAMILIA YANGU

Familia yangu ina baba, mama, mimi na ndugu zangu; wawili wa kike na wawili wa kiume. Kiongozi wa familia yangu ni baba. Yeye ni mwalimu katika shule jirani. Baba yangu ni mtu mzuri sana lakini ukimkasirisha,  utapata adhabu. Huwa anafanya kazi kwa bidii ili kukimu mahitaji ya familia yetu. Yeye hutununulia chakula, hutulipia karo, na hutununulia nguo. Zaidi ya yote, anaipenda familia yake sana.

Mama yangu ni msaidizi wa baba. Yeye ni nesi na anafanya kazi kwenye hospitali moja karibu na kwetu. Yeye ni mpole na mwenye bidii. Wakati mwingi, huwa hayuko nyumbani. Lakini anahakikisha anapata muda wa kukaa na familia yake. Yeye hutupa moyo hasa kuhusu shughuli za kiakademia, na anachukizwa sana na uvivu na utovu wa nidhamu. Mama yangu anaweza kumwadhibu yeyote kwa kutumia kifaa chochote anapokasirika. Kabla ya kumwadhibu mtu, yeye  humweleza makosa na baadaye kumwadhibu.

Wikendi, wazazi wangu huwa nyumbani. Sote tunasaidia kufanya kazi za nyumbani na shambani. Tunaweza kupanda mbegu za mimea mbalimbali au kupalilia mimea.

Siku za Jumapili, baada ya kula kiamshakinywa,  sote huelekea kanisani. Wazazi wetu hutufunza kwamba, ni vyema kutenga muda wa Mungu. Tukienda kanisani, huwa wanatuhimiza kumtolea Mungu sadaka. Baada ya hapo, huwa tunatembelea makao ya watoto yatima. Tunawapelekea nguo na vyakula. Watoto yatima hukosa mapenzi ya wazazi, kwa hivyo, tukiwaonyesha upendo, wanapata moyo wa kuishi kwa furaha kama watoto wengine wenye wazazi.

Wakati wa likizo, huwa tunawatembelea babu na bibi nyumbani kwao. Sisi hunawapelekea vitu mbalimbali na kukaa nao kwa siku kadhaa. Wanafurahi sana wakati wajukuu wao wanawatembelea. Wao hutupatia mafunzo mengi kupitia hadithi na mazungumzo ya kawaida. 

Thursday, 9 February 2023

-OTE & -O-OTE [ALL & ANY]

-ote             [all, the whole]

-o-ote         [any, whichever, whatsoever]


Expressing all with personal pronouns

sisi sote

[all of us]

nyinyi nyote

[all of you]

wao wote

[all of them]

 

 Expressing all or any with other noun classes

Class

-ote

-o-ote

Singular

Plural

Singular

Plural

M-WA

-

wote

yeyote

wowote

KI-VI

chote

vyote

chochote

vyovyote

M-MI

wote

yote

wowote

yoyote

JI-MA

lote

yote

lolote

yoyote

U

wote

zote

wowote

zozote

N

yote

zote

yoyote

zozote

KU

kote

kote

kwokwote

kwokwote

PA-KU-MU

pote

pote

pokote

pokote

 

Kote

Kote

 

Kokote

kokote

 

 Mifano [Examples] 

1.     Sisi sote tutaenda kesho [All of us will go tomorrow]

2.     Watu wote wameenda [All people have gone]

3.     Hakuna mtu yeyote ameenda [No person whatsoever has left]

4.    Kitambaa chote ni cheusi [The whole cloth is black]

5.     Nipatie kitambaa chochote [Give me any cloth]

6.      Ukuta wote umebomoka [The whole wall has collapsed]

7.      Nimetafuta mahali pote [I searched everywhere]

8.    Huendi mahali popote [You are not going anywhere]

 

 

Zoezi [Exercise]: Translate into Kiswahili

a)    All people need love.

b)    Anybody can open the door.

c)     All hotels are closed, and none are open.

d)   All rooms are open, you can use any.

e)    I did not ask any questions.

f)      All walls are red, and none is white.

g)    I like all types of food.

h)   He wanted to talk to anyone.

i)      Did you see all the houses?

j)      Did you have any problems?