PESA NA UNUNUZI
Pesa/fedha |
Money |
Nunua |
Buy |
Uza |
Sell |
Mteja |
Customer |
Mnunuzi |
Buyer |
Muuzaji |
Seller |
Bei |
Cost/price |
Kujadiliana bei |
To bargain |
Duka |
Shop |
Baki/Salio |
Change |
Shilingi |
Shillings |
Biashara |
Business |
Soko (ni) |
(at the) market |
Punguza bei |
Reduce the price |
Ni pesa ngapi/ Ni bei gani |
How much is the price |
Lipa |
Pay |
Bei rahisi |
Cheap |
Bei ghali |
Expensive |
Mazungumzo
Mnunuzi: Habari
ya mchana?
Muuzaji: Salama,
nashukuru.
Mnunuzi: Nimependa
viatu hivi, unauza shilingi ngapi?
Muuzaji: Nauza
shilingi elfu tano.
Mnunuzi: Elfu
tano? Hiyo ni ghali sana.
Muuzaji: Una
shilingi ngapi mteja wangu?
Mnunuzi: Nina
elfu mbili mia tano, hiyo ndiyo bajeti yangu.
Muuzaji: Hiyo ni
kidogo sana, unaweza kuongeza ngapi?
Mnunuzi: Kusema
kweli, nina hiyo tu, au labda niongeze shilingi mia tano.
Muuzaji: Hiyo ni
afadhali, naona tunaweza kuelewana.
Mnunuzi: (Akitabasamu)
Hivyo nikupatie shilingi ngapi?
Muuzaji: Ningependa
uongeze mia mbili ili nitengeneze faida.
Mnunuzi: (Akicheka) Najua utapata faida nyingi hata kwa hiyo bei.
Muuzaji: Hapana hata! Bei niliyoinunua ni
elfu tatu mia mbili, hivyo nikiuza elfu tatu nitapata hasara na biashara yangu itakuwa
hatarini. Nikutafutie viatu vingine vya shilingi elfu tatu?
Mnunuzi: Hapana! Hivi ndivyo nilivyopenda. Singependa
kuangusha biashara yako lakini pia usiniwekee bei ya juu zaidi. Hivyo, utakubali
elfu tatu mia tano?
Muuzaji: Nitashukuru
angalau nitakuwa na faida.
Mnunuzi: Sawasawa,
nitashukuru. (Anampa muuzaji shilingi elfu
nne).
Muuzaji: Asante
mteja wangu.
Mnunuzi: Karibu.
Lakini usisahau kunipa baki langu. Itakuwa shilingi mia tano.
Muuzaji: (Anatoa baki ya
shilingi mia tano na kumpatia mteja) Asante sana na karibu tena.
Mnunuzi: Asante.
Buyer: Good
afternoon?
Seller: I’m
fine, thank you.
Buyer: I
like these shoes, how much do they cost?
Seller: They
cost five thousand shillings.
Buyer: Five
thousand? That is too expensive.
Seller: How
much do you have my customer?
Buyer: I
have two thousand five hundred shillings, that is my budget.
Seller: That
is too little, how much can you add?
Buyer: To
be honest, that’s all I have. Maybe I could add five hundred shillings.
Seller: That's
better, I see we can come to an agreement.
Buyer: (Smiling) So how much should I give you?
Seller: I
would like you to add an extra two hundred shillings so that I can make a
profit.
Buyer: (Laughing) I know you will still make a lot of profit at that price.
Seller: Not at all! My buying price was three thousand two
hundred, so if I sell at three thousand, I will incur a loss and my business
will be in trouble. Could I get you a different pair of shoes that costs three
thousand shillings?
Buyer: No!
This is what I liked. I would not like to bring down your business but also do
not set a high price for me. So, will you accept three thousand five hundred
shillings?
Seller: I
will be grateful at least I will make some profit.
Buyer: Okay,
thank you. (He gives four thousand
shillings to the seller).
Seller: Thank
you my customer.
Buyer: Welcome.
But don't forget to give me my balance. It will be five hundred shillings.
Seller: (He gives the change of five hundred shillings to the customer) Thank you
very much and welcome again.
Buyer: Thank
you
Useful phrases to use when you go shopping.
Ninataka kununua
machungwa. |
I want to buy oranges. |
Punguza bei
kidogo. |
Come down a little on the price. |
Mbona ghali
sana? |
Why so expensive? |
Ninaweza kulipa
kwa kadi? |
May I pay by card? |
Sina pesa
taslimu. |
I do not have cash. |
Exercise 1
Mtu anayenunua bidhaa dukani anaitwaje?
Muuzaji
Mnunuzi
Mkulima
Duka
Mtu anayeuza bidhaa anaitwaje?
Mkuu
Mnunuzi
Mkulima
Muuzaji
Mtu anapouliza “shilingi ngapi?” anamaanisha nini?
Bei ya bidhaa
Baki yangu
Bajeti
Biashara
How do you ask for the cost of a product?
Bidhaa hiyo ni shilingi ngapi?
Bidhaa hiyo inapatikana wapi?
Bidhaa hiyo ni gani?
Ninataka bidhaa hiyo
Translate: Baki
Change
Cost
Deni
Pesa
Translate to Kiswahili: I will go shopping today.
Nitaenda kununua bidhaa leo.
Nitauza bidhaa leo.
Nanunua duka leo.
Nakuja kununua bidhaa.
Utatumia nini kununua bidhaa?
Karatasi
Kitabu
Pesa
Mikono
Translate to English: Kikombe hicho ni ghali.
That cup is expensive.
The cup is cheap.
The cup is there.
This is a cup.
Translate to Kiswahili: I am going to the market.
Ninaenda dukani.
Ninaenda sokoni.
Naenda matembezi.
Ameenda kununua bidhaa.
Budget katika Kiswahili inaitwaje?
Orodha
Bei
Bajeti
Riba
Translate to Kiswahili: She bought a book.
Alinunua kitabu.
Aliuza kitabu.
Alitoa kitabu.
Alinipatia kitabu.
Supermarket katika Kiswahili inaitwaje?
Duka
Soko
Duka kubwa
Duka la dawa
Translate to Kiswahili: Cheap
Bidhaa ghushi
Ghali
Rahisi
Bidhaa ya bei
Translate to English: Duka
Soko
Shop
Market
Bank
Interest inaitwaje katika Kiswahili?
Baki
Riba
Chenji
bei
Exercise 2
Translate the following to Kiswahili.
- Price
- How much
- Customer
- Seller
- Sell
- Buy
- Expensive
- Please reduce the
price