Pages

Thursday, 10 February 2022

Shopping

 PESA NA UNUNUZI

 

Pesa/fedha

Money

Nunua

Buy

Uza

Sell

Mteja

Customer

Mnunuzi

Buyer

Muuzaji

Seller

Bei

Cost/price

Kujadiliana bei

To bargain

Duka

Shop

Baki/Salio

Change

Shilingi

Shillings

Biashara        

Business

Soko (ni)

(at the) market

Punguza bei

Reduce the price

Ni pesa ngapi/ Ni bei gani

How much is the price

Lipa

Pay

Bei rahisi

Cheap

Bei ghali

Expensive

 

 

 

 

Mazungumzo

 

Mnunuzi:    Habari ya mchana?

Muuzaji:      Salama, nashukuru.

Mnunuzi:    Nimependa viatu hivi, unauza shilingi ngapi?

Muuzaji:      Nauza shilingi elfu tano.

Mnunuzi:    Elfu tano?  Hiyo ni ghali sana.

Muuzaji:      Una shilingi ngapi mteja wangu?

Mnunuzi:    Nina elfu mbili mia tano, hiyo ndiyo bajeti yangu.

Muuzaji:      Hiyo ni kidogo sana, unaweza kuongeza ngapi?

Mnunuzi:    Kusema kweli, nina hiyo tu, au labda niongeze shilingi mia tano.

Muuzaji:      Hiyo ni afadhali, naona tunaweza kuelewana.

Mnunuzi:    (Akitabasamu) Hivyo nikupatie shilingi ngapi?

Muuzaji:      Ningependa uongeze mia mbili ili nitengeneze faida.

Mnunuzi:    (Akicheka) Najua utapata faida nyingi hata kwa hiyo bei.

Muuzaji:      Hapana hata! Bei niliyoinunua ni elfu tatu mia mbili, hivyo nikiuza elfu tatu nitapata hasara na biashara yangu itakuwa hatarini. Nikutafutie viatu vingine vya shilingi elfu tatu?

Mnunuzi:    Hapana! Hivi ndivyo nilivyopenda. Singependa kuangusha biashara yako lakini pia usiniwekee bei ya juu zaidi. Hivyo, utakubali elfu tatu mia tano?

Muuzaji:      Nitashukuru angalau nitakuwa na faida.

Mnunuzi:    Sawasawa, nitashukuru. (Anampa muuzaji shilingi elfu nne).

Muuzaji:      Asante mteja wangu.

Mnunuzi:    Karibu. Lakini usisahau kunipa baki langu. Itakuwa shilingi mia tano.

Muuzaji:      (Anatoa baki ya shilingi mia tano na kumpatia mteja) Asante sana na karibu tena.

Mnunuzi:    Asante.



Buyer:                 Good afternoon?

Seller:                   I’m fine, thank you.

Buyer:                 I like these shoes, how much do they cost?

Seller:                   They cost five thousand shillings.

Buyer:                 Five thousand? That is too expensive.

Seller:                   How much do you have my customer?

Buyer:                 I have two thousand five hundred shillings, that is my budget.

Seller:                   That is too little, how much can you add?

Buyer:                 To be honest, that’s all I have. Maybe I could add five hundred shillings.

Seller:                   That's better, I see we can come to an agreement.

Buyer:                 (Smiling) So how much should I give you?

Seller:                   I would like you to add an extra two hundred shillings so that I can make a profit.

Buyer:                 (Laughing) I know you will still make a lot of profit at that price.

Seller:                   Not at all! My buying price was three thousand two hundred, so if I sell at three thousand, I will incur a loss and my business will be in trouble. Could I get you a different pair of shoes that costs three thousand shillings?

Buyer:                  No! This is what I liked. I would not like to bring down your business but also do not set a high price for me. So, will you accept three thousand five hundred shillings?

Seller:                   I will be grateful at least I will make some profit.

Buyer:                 Okay, thank you. (He gives four thousand shillings to the seller).

Seller:                   Thank you my customer.

Buyer:                 Welcome. But don't forget to give me my balance. It will be five hundred shillings.

Seller:                   (He gives the change of five hundred shillings to the customer) Thank you very much and welcome again.

Buyer:                 Thank you

 

Useful phrases to use when you go shopping.

Ninataka kununua machungwa.

I want to buy oranges.

Punguza bei kidogo.

Come down a little on the price.

Mbona ghali sana?

Why so expensive?

Ninaweza kulipa kwa kadi?

May I pay by card?

Sina pesa taslimu.

I do not have cash.

                       

 

Exercise 1

Mtu anayenunua bidhaa dukani anaitwaje?

Muuzaji

Mnunuzi

Mkulima

Duka


Mtu anayeuza bidhaa anaitwaje?

Mkuu

Mnunuzi

Mkulima

Muuzaji


Mtu anapouliza “shilingi ngapi?” anamaanisha nini?

Bei ya bidhaa

Baki yangu

Bajeti

Biashara


How do you ask for the cost of a product? 

Bidhaa hiyo ni shilingi ngapi?

Bidhaa hiyo inapatikana wapi?

Bidhaa hiyo ni gani?

Ninataka bidhaa hiyo


Translate: Baki

Change

Cost

Deni

Pesa


Translate to Kiswahili: I will go shopping today. 

Nitaenda kununua bidhaa leo.

Nitauza bidhaa leo.

Nanunua duka leo.

Nakuja kununua bidhaa.


Utatumia nini kununua bidhaa?

Karatasi

Kitabu

Pesa

Mikono


Translate to English: Kikombe hicho ni ghali. 

That cup is expensive. 

The cup is cheap.

The cup is there. 

This is a cup. 


Translate to Kiswahili: I am going to the market. 

Ninaenda dukani.

Ninaenda sokoni.

Naenda matembezi.

Ameenda kununua bidhaa.


Budget katika Kiswahili inaitwaje? 

Orodha

Bei

Bajeti

Riba


Translate to Kiswahili:  She bought a book. 

Alinunua kitabu.

Aliuza kitabu.

Alitoa kitabu.

Alinipatia kitabu.


Supermarket katika Kiswahili inaitwaje? 

Duka

Soko

Duka kubwa

Duka la dawa


Translate to Kiswahili: Cheap 

Bidhaa ghushi

Ghali

Rahisi

Bidhaa ya bei


Translate to English: Duka 

Soko

Shop 

Market 

Bank 


Interest inaitwaje katika Kiswahili? 

Baki

Riba

Chenji

bei


Exercise 2

Translate the following to Kiswahili.

    1. Price
    2. How much
    3. Customer
    4. Seller
    5. Sell
    6. Buy
    7. Expensive
    8. Please reduce the price

 

No comments:

Post a Comment

Please leave your comment/question or suggestion.