Nchi zetu za Afrika zinakumbwa sana na ukosefu wa mvua. Inasemekana ya kwamba jangwa linazidi kutanda katika bara hili, kwa hivyo ni wajibu wetu kujiandaa na kuchukua hatua kadha wa kadha ili tuweze kupambana na ukavu huu, kwani wahenga walisema, “Uwahi udongo uli maji.”
Kwa hakika ukavu huu unasambaa katika bara hili na unatutia
hofu kubwa. Imekuwa sana tunategemea nchi za kigeni kutusaidia. Tukichunguza
zaidi sababu kubwa ya ukosefu wa mvua ya kutosha ni ukataji wa miti. Kwa hivyo
tuhakikishe kuwa tutapanda miti kwa wingi wakati wa mvua. Serikali ya Kenya
inahimiza sana upandaji wa miti katika sehemu mbalimbali za nchi. Pia lazima
tuhakikishe kwamba baada ya mche kupandwa, kufanywe mipango na kupatikane watu
ambao wataiangalia na kuipalilia hadi itakapokuwa mkubwa. Ni wazi kwamba
tumetilia mkazo wa kupanda miche lakini hatujazingatia miche hii kuangaliwa kwa
kunyunyiziwa maji wakati wa ukame.
Hatua ya kuchimba visima, katika sehemu zenye ukavu ni jambo
la muhimu sana, kwani maji ya visima yataweza kutumika majumbani na pia
kunyunyizia mimea. Maji kwa binadamu ni kitu muhimu sana kwa sababu bila ya
maji hakuna uhai. Huko Australia, visima vingi vimechimbwa katika sehemu zenye
ukame kwa minajili ya kuwapatia wakazi wa sehemu hizo maji ya nyumbani, mifugo
na kunyunyizia mimea.
Maji ya mvua na yale yanayochuruzika mitaroni, hukusanywa na
kutumiwa kwa kunyunyizia mimea. Mashamba yanayonyunyuziwa maji ya aina hii,
hunawiri na kustawi sana. Maji ya mito ambayo huchuruzika baharini, lazima
tuyatumie baada ya kuiondoa chumvi ndani yake. Vile dana, tujaribu tuwezavyo
kupanda mimea ambayo itatupa chakula cha kutosha ili tuweze kujitegemea badala
ya kuzitegemea nchi za kigeni.
(a) Mwandishi ametumia methali “uwahi udongo uli maji”
akimaanisha nini hasa?
(b) “Haitoshi tu kupanda miche na kutulia”. Kulingana na
yaliyomo katika taarifa hii, ni hatua gani zingine zinazohitajika ili kufaulu
katika mradi huo wa upanzi?
(c) Taja jitihada zozote mbili zinazochukuliwa na serikali ili
kukabiliana na shida ya ukosefu wa mvua / maji.
(d) Kwa nini maji ya baharini hayatumiwi moja kwa moja?
(e) Kwa nini nchi nyingi za bara la Afrika zinategemea nchi za
kigeni?
(f) Maneno yafuatayo yametumiwa kuleta maana gani?
(i) Kutanda____________________________
(ii) Miche_____________________________
(iii) Kunyunyizia________________________
(iv) Hunawiri__________________________
(v) Kustawi___________________________
No comments:
Post a Comment
Please leave your comment/question or suggestion.